1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Rafael Grossi kufanya ziara Iran kuhusu mpango wa nyuklia

13 Novemba 2024

Mkuu wa shirika la kimataifa la kudhibiti matumizi ya nishati ya nyuklia Rafael Grossi, anatazamiwa kuwasili nchini Iran.

Rafael Grossi atarajiwa kuzuru Iran tena.
Rafael Grossi atarajiwa kuzuru Iran tena.Picha: Tasnim

Ziara ya Grossi nchini Iran ni kwa ajili ya mazungumzo muhimu kuhusu mpango wa nyuklia wa nchi hiyo akitahadharisha kwamba uwezekano ya kufikia mapatano unazidi kupungua.

Grossi anafanya ziara hiyo siku mbili tu baada ya waziri wa ulinzi wa Israel kusema kuwa vituo vya nyuklia vya Iran vinaweza kushambuliwa.

Mkuu huyo wa shirika la kimataiafa la nishati ya nyuklia amesisitiza kuwepo uwazi juu ya mipango ya nyuklia ya Iran.

Amesema Iran inazo nyenzo za kutosha kwa ajli ya kuunda silaha za nyuklia ingawa ameeleza kwamba kwa sasa Iran haina silaha hizo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW