Raia 2 wauawa Afghanistan katika shambulizi la kujitolea muhanga
15 Machi 2008Matangazo
KABUL:
Nchini Afghanistan,raia 2 wameuawa katika shambulizi la kujitolea muhanga.Mwanajeshi mmoja wa vikosi vya madola shirika,alijeruhiwa pia.Mshambulizi alibamiza gari lake katika msafara wa magari ya kijeshi ya NATO.Shambulio hilo limetokea karibu na mji wa Shost ulio kusini mashariki mwa Afghanistan karibu na mpaka wa Pakistan.