1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Ugaidi

Raia 20 wauwa kaskazini-mashariki mwa DRC

18 Mei 2020

Wanawake na watoto walikuwa miongoni mwa raia wasiopungua 20 waliouawa katika mkoa wa kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo wa Ituri, wamesema maafisa wa serikali siku ya Jumapili.

Demokratische Republik Kongo Soldaten Patroullie nahe Beni
Picha: picture-alliance/AP Images/Al-Hadji Kudra Maliro

Hali ya usalama inaendelea kuwa mbaya katika maeneo mbalimbali ya mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Katika mji mdogo wa Kokola kwenye mkoa wa Kivu ya Kaskazini, waasi kutoka Uganda wa kundi la ADF waliwauwa watu saba na kuzichoma moto nyumba kadhaa. Na katika wilaya ya Djugu mkoani Ituri, watu 20 wameuawa na waasi wa CODECO.

Mashambulizi haya yanayoshuhudiwa mara kwa mara yamewakatisha tamaa wakaazi wa wilaya ya Beni katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini, na wakaazi wa wilaya ya Djugu katika mkoa wa Ituri. 

Katika wilaya ya Beni, mashirika ya kiraia yametangaza kuwa watu wasiopungua thelathini wameuawa na waasi wa ADF, katika kipindi cha wiki moja.

Rais wa DRC Felix TshisekediPicha: G. Kusema

Kundi la CODECO linashutumiwa kwa mauaji ya mamia ya raia katik mwaka huu pekee. Wanachama wake wantokea kundi la kabila la Lendu, ambao kwa sehemu kubwa ni wakulima, na wanapambana mara kwa mara na jamii ya w Hema ambao ni wafanyabiashara na wafugaji mkoani Ituri - mkoa wensye utajiri mkubwa wa dhahbu na mafuta.

Kwa taifa zima, idadi ya wahanga kutokana na vurugu za kikabila inakaribia 1,000 tangu Desemba 2017. Kwa mujibu wa shirika la wakimbizi duniani, UNHCR Mei 8, idadi ya mwaka huu ilikuwa siyo chini ya watu 274 waliouawa na 200,000 wamekimbia vurugu.

Siku ya Jumapili, shambulio lilidhihirika kutoka eneo la Walendu wakati wahanga walikuwa watu wa kabila la Hema, kilisema chanzo kutoka eneo hilo.

Katika eneo la Djugu, lenye ukubwa wa zaidi ya kilomita 8,000 za mraba (maili za mraba 3,000), vijiji kutoka makundi yote mawili vimechanganyika na msemaji wa jeshi Jules Ngongo aliliambia shirika la habari la afp: "Hakuna jeshi duniani kote linaweza kila mahalala katika kanda kama Djugu.

Kombania mbili za Umoja wa Mataifa zilipelekwa pia kwenye mkoa huo, na zinasaidiwa na wanajeshi wa kikosi maalumu cha Uruguay, ulisema ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, MONUSCO mwishoni mwa Aprili.

Mamia kwa maelf waliuawa katika eneo hilo kati ya 1999 na 2003. Umoja wa Mataifa unasema wahanga wengi walilengwa kwa sababu walikuwa wa kabila la Hema.

Chanzo: afpe