1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Washambuliaji wawauwa raia kadhaa wa Sudan

21 Juni 2023

Raia kadhaa wa Sudan wameuwawa kwa kushambuliwa au kupigwa risasi wakati wakajaribu kuukimbia mji wa El Geneina uliopo katika jimbo la Darfur.

Konflikt im Sudan
Picha: AP/picture alliance

Mashuhuda  waliozungumza na shirika la habari la Reuters, wamesema wengi ya waliouwawa walikuwa wanakimbia machafuko yanayoukumba mji huo na taifa la Sudan kwa jumla wakilenga kuingia nchi jirani ya Chad.

Washambuliaji huwafyetulia risasi watu wanaotoroka 

Kulingana na mashuhuda, makundi ya watu wenye silaha huwavizia na kuwafyetulia risasi watu wanaotoroka mji huo kwa mguu, kuelekea mji wa Adre nchini Chad kiasi kilometa 27 kutoka El Geneina.

Machafuko ya kiasi miezi miwili kwenye mji wa El Geneina yamekuwa yakifanywa zaidi na  makundi ya wanamgambo wa makabila ya kiarabu pamoja na wapiganaji wa kikosi chenye nguvu cha RSF kinachopambana na jeshi ya taifa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW