1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia kumi wauawa kwenye mashambulio ya anga Sudan

6 Januari 2025

Raia kumi wa Sudan wameuawa kwenye shambulio la anga la vikosi vya anga kusini mwa mji mkuu Khartoum. Waokoaji wamesema zaidi ya watu 30 walijeruhiwa.

Sudan Omdurman | Zerstörungen nach Bombardierung
Watu wanapita karibu na gari lililoharibiwa, kufuatia kushambuliwa kwa makombora na Vikosi vya RSF, huko Omdurman, Sudan, Desemba 10, 2024.Picha: Khartoum State Government/REUTERS

Mtandao wa wafanyakazi wa dharura wa kujitolea, ERR wanaoratibu maafa katika eneo la mstari wa mbele wa vita umesema mashambulio hayo yalilenga soko katika Ukanda wa Kusini mwa mji mkuu mara tatu katika muda wa chini ya mwezi mmoja. Kundi hilo limesema watu waliofikwa na maafa hayo waliuawa kwa kuchomwa moto na waliojeruhiwa wanaugua majeraha ya moto katika hospitali ya Bashair huku watano kati yao wakiwa katika hali mahututi. Tangu mwezi Aprili mwaka 2023, vita kati ya jeshi kuu la Sudan na kikosi cha (RSF) vimesababisha vifo vya maelfu ya watu. Wasudan milioni 11.5 wamegeuka wakimbizi wa ndani na wengine wameikimbia nchi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW