1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBangladesh

Raia wa Bangladesh wapiga kura tangu vuguvugu la 2024

12 Februari 2026

Raia wa Bangladesh wanapiga kura leo katika uchaguzi mkuu tangu kulipofanyika maandamano makubwa ya mwaka 2024 yaliyoratibiwa na vijana yaliyomuondoa madarakani Waziri Mkuu Sheikh Hasina.

Bangladesh Dhaka 2026 | 13. Uchaguzi wa wabunge na kura ya maoni - wapiga kura wamepanga foleni katika kituo cha kupigia kura
Raia wa Bangladesh wanapiga kura kwenye uchaguzi mkuu tangu taifa hilo lilipogubikwa na maandamano yaliyomuondoa madarakani Waziri mkuu Sheikh Hasina, 2024Picha: Abdul Goni/Anadolu Agency/IMAGO

Usalama umeimarishwa kote nchini humo wakati uchaguzi huo pamoja na kura ya maoni kuhusu mageuzi ya katiba vikiendelea, ambapo vikosi vya usalama zaidi ya 900,000 vikiwa vimesambazwa.

Mamlaka zimesema zinataka kuhakikisha kunakuwepo na usalama katika kila hatua katikati ya hali tete ya kisiasa chini Bangladesh.

Mkuu wa Tume ya Uchaguzi Nasir Uddin amezihimiza pande zinazohasimiana na wapiga kura kulitekeleza zoezi hilo kwa utulivu na kukubali matokeo, licha ya tofauti za maoni.

Mshauri wa Mambo ya Ndani Jahangair Alam Chowdhury ameonya hatua kali zinaweza kuchukuliwa dhidi ya jaribio lolote la kuvuruga uchaguzi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW