1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wa Finland wapiga kura ya urais

28 Januari 2024

Raia nchini Finland wanapiga kura hii leo kuanza mchakato wa kumchagua kiongozi wa nchi hiyo.

Uchaguzi wa rais Finland
Mpiga kura akipiga kura wakati wa uchaguzi wa rais katika shule ya Friisila huko Espoo, Finland.Picha: Mikko Stig/AFP

Wagombea tisa wanawania nafasi hiyo ili kujaza nafasi ya Rais Sauli Niinisto, mwenye miaka 75 anayetakiwa kuondoka madarakani baada ya kukaa madarakani kwa mihula miwili.

Soma pia: Finland nchi yenye furaha zaidi duniani

Takriban raia milioni 4.5 wenye sifa, wanatarajiwa kupiga kura. Awali kura za maoni zilionesha kuwa mgombea wachama cha kihafidhina Alexander Stubb, na waziri wa zamani wa mambo ya kigeni Pekka Haavisto chama cha kijani wanapewa nafasi kubwa kwenye kinyang'anyiro hicho.

Soma pia: Putin aitisha Finland kufuatia hatua yake ya kujiunga na jumuiya ya kujihami ya NATO

Matokeo ya awali yanatarajiwa kufahamika Jumapili jioni. Ikiwa hakuna mgombea atakayepata zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo, wagombea wawili wwaliopata kura nyingi zaidi wataingia katika awamu ya pili ndani ya wiki mbili.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW