1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wa Guinea Bissau wapiga kura kumchagua rais mpya

23 Novemba 2025

Raia katika taifa dogo la Afrika Magharibi la Guinea Bissau ambalo limeshuhudia mapinduzi mengi ya kijeshi, wanapiga kura hii leo kumchagua rais mpya.

Guinea-Bissau 2025 | Uchaguzi wa rais na bunge
Raia wa Guinea Bissau wanapiga kura wakitumai kufungua kurasa mpya za kisiasa, licha ya chama kikuu cha upinzani kunyimwa nafasi ya kushiriki.Picha: Iancuba Dansó/DW

Raia wa taifa hilo wanatumai kufungua kurasa mpya za kisiasa, licha ya chama kikuu cha upinzani kunyimwa nafasi ya kushiriki.

Takriban wapiga kura 860,000 wanashiriki uchaguzi huo mkuu ulio na wagombea 12, huku suala la uthabiti wa taifa likiwa ndilo linalowavutia wapiga kura wengi wanaotaka kuiona nchi hiyo ikiwa imara, baada ya kukumbwa na migogoro mingi ya kisiasa tangu ilipopata uhuru wake kutoka Ureno zaidi ya miaka 50 iliyopita.

Rais anayetetea kiti chake Umaro Sissoco Embalo, aliye na umri wa miaka 53 anatarajiwa kushinda. Mpinzani wake mkuu Fernando Dias, hakugombea kufuatia mahakama kuu nchini humo kusema maombi yake ya kushiriki hayakufika kwa wakati.

Raia wa Guinea Bissau wanataka rais ajae aimarishe hali ya maisha, ikiwemo huduma bora za afya, elimu, miundombinu, mageuzi ya kisiasa na njia za kukabiliana na umasikini. Matokeo ya Uchaguzi huo yanatarajiwa kutolewa siku ya Alhamisi wiki ijayo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW