1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wa Kongo zaidi ya 2000 waomba hifadhi Tanzania

Admin.WagnerD15 Machi 2023

Zaidi ya raia 2000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameingia nchini Tanzania kuomba hifadhi ya ukimbizi kufuatia machafuko yanayoendelea katika mikoa ya mashariki.

Grenze DR Kongo Uganda Bunagana Flüchtlinge
Picha: Guerchom Ndebo/AFP/Getty Images

Kwa mujibu wa idara ya wakimbizi ya wizara ya mambo ya ndani nchini Tanzania wakimbizi hao wameanza kuingia nchini Machi 05 mwaka huu.

Idara hiyo imeongeza kwamba kwa wastani wanapokelewa kati ya watu mia moja hadi 300 kila siku.

 Mkurugenzi wa idara ya wakimbizi nchini Tanzania Bw. Sudi Mwakibasi amesema kinachofanyika kwa sasa, ni Tanzania kutekeleza hitaji la msingila kuwapokea wanaohitaji hifadhi.

 "Hadi leo tumepokea waomba hifadhi 2,643."Alisema bwana Mwakibasi

Aliongeza kwamba kati ya hao, takriban 630 tayari wamehojiwa ili kuthibitisha uhalali wao na kupewa hifadhi katika kambi ya Nyarugusu mkoani Kigoma magharibi mwa taifa hilo la Afrika mashariki.

Soma pia:Usalama wazidi kuzorota nchini Kongo

 Mamamalaka nchini humo zimeongeza kwamba  kundi hilo linahusisha wakimbizi wapya walioingia moja kwa moja kutoka DRC pamoja na waliokuwa wakiishi nchini  bila vibali.

 Kutetereka hali ya usalama kumechangia 

Waomba hifadhi hao wameiambia DW kuwa kinachowaondoa Kongo ni ongezeko la mashambulizii ya waasi wa kundi la M23 wanaokabiliana na majeshi ya serikali. 

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye akiongea na waomba hifadhi hao ambao awali walipokelewa na kanisa katolikiamewataka kuwa watulivu wakati suala lao likishughulikiwa.

Soma pia:Zaidi ya watu 70 wauwawa na ADF Kongo

Aidha ametoa onyo kwa waomba hifadhi hao akiwataka kutoa taarifa za kweli wanapohitajika kufanya hivyo huku akitoa onyo kwa wenyeji kuwa watulivu wakatio huu.

 Mkoa wa Kigoma hadi sasa unahifadhi wakimbizi wapatao laki mbili kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na Jamhurii ya Burundi.

Ukimbizi shida DRC

01:12

This browser does not support the video element.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW