1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Liberia wapiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais

Sylvia Mwehozi
14 Novemba 2023

Raia wa Liberia wanapiga kura hii leo katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais, huku mwanasoka wa zamani George Weah akitafuta kuchaguliwa kwa muhula wa pili madarakani.

Uchaguzi Liberia 2023
Wapigakura nchini Liberia wakishiriki zoezi la kumchagua rais katika duru ya kwanza iliyofanyika Oktoba 10, 2023.Picha: John Wessels/AFP

Wagombea wote wawili walichuana vikali mwaka 2017 wakati Weah aliposhinda katika raundi ya pili kwa zaidi ya asilimia 61 ya kura. Uchaguzi huo unafanyika baada ya kutopatikana mshindi katika awamu ya kwanza ya Oktoba 10.

Matokeo ya duru ya kwanza ya upigaji kura mwezi uliopita yanaonyesha kukaribiana sana kwa wagombea hao: George Weah alipata asilimia 43.83 huku Joseph Boakai akijikingia asilima 43.44 ya matokeo jumla.

Soma pia: Waangalizi wa kimataifa waipongeza Liberia kwa uchaguzi wake

Uchaguzi wa mwaka huu ni wa kwanza tangu Umoja wa Mataifa ulipohitimisha ujumbe wa kulinda amani nchini Liberia.Ujumbe huo uliundwa baada ya zaidi ya watu 250,000 kufariki katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka 1989 na 2003.

Waangalizi wanasisitiza umuhimu wa kudumisha amani na kukubali matokeo rasmi ya tume ya uchaguzi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW