Mbaroni kwa kupanga mashambulizi dhidi ya ubalozi wa Israel
20 Oktoba 2024Matangazo
Kulingana na gazeti la kila siku la Bild, kikosi maalumu cha polisi kilivamia makazi ya kijana huyo mwenye miaka 28 siku ya Jumamosi nje kidogo mwa mji mkuu Berlin na kumtia nguvuni.
Soma zaidiPolisi mjini Munich wamuua mshukiwa wa 'ugaidi' karibu na ubalozi wa Israel:
Gazeti hilo limeeleza kuwa polisi walichukua hatua hiyo baada ya kupewa taarifa na shirika la kijasusi la nchi nyingine na kuwa mtuhumiwa hakuwa katika orodha ya kundi lolole linalofuatiliwa na polisi nchini Ujerumani.
Kijana huyo anadhaniwa kuwa aliingia Ujerumani Novemba mwaka 2022 na kuomba hifadhi mwezi Januari mwaka uliofuata, ombi ambalo hata hivyo lilikataliwa Septemba 2023.