1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

Raia wa Mali wakabiliana na maisha magumu tangu mapinduzi

19 Agosti 2024

Wakazi wengi wa Mali wamelalamika kuwa hali inazidi kuwa mbaya nchini humo, miaka minne tangu yafanyike mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa madarakani rais wa wakati huo Ibrahim Boubacar Keita.

Takriban asilimi 90 ya wakazi wa Mali wanaishi katika umaskini.
Takriban asilimi 90 ya wakazi wa Mali wanaishi katika umaskini.Picha: EPA/dpa/picture alliance

Raia hao wamesema tangu mapinduzi ya mwaka 2020, kunashudiwa ongezeko la matatizo ya kiusalama, kiuchumi na pia tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara jambo linaloathiri shughuli za biashara.

Tathmini ya Benki ya Dunia imeonyesha kuwa ukuaji wa uchumi wa Mali unatarajiwa kupungua hadi asilimia 3.1 mwaka huu kutoka asilimia 3.5 mwaka jana, huku viwango vya juu vya umaskini vikiongezeka.

Takriban asilimi 90 ya wakazi wa Mali wanaishi katika umaskini.