1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wa Marekani afungwa miaka 15 jela Urusi

24 Desemba 2024

Raia mmoja wa Marekani mwenye asili ya Urusi amehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela baada ya kushitakiwa kwa madai ya ujasusi.

Moscow
Raia wa Marekani aliye na asili ya Kirusi afungwa miaka 15 jela kwa madai ya kijasusiPicha: Anton Novoderezhkin/TASS/picture alliance

Shirika la habari la Interfax limesema Gene Spector ambaye tayari amekuwepo kizuizini kwa muda alikuwa mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya vifaa vya matibabu. 

Kesi hiyo imeendeshwa kwa faragha katika mahakama moja mjini Moscow na hakuna mashitaka mengine dhidi ya mwanamume huyo yaliyotolewa hadharani. 

Urusi yamfunga jela mwandishi habari wa Marekani Kurmasheva

Spector tayari alikuwa ameshitakiwa kwa masuala ya ufisadi mwaka 2022, kwa mdai ya kuwa sehemu ya rushwa iliyokuwa ilipwe kwa mfanyakazi wa zamani wa aliyekuwa naibu waziri Mkuu wa Urusi Arkady Dvorkovich. Kwa kosa hilo alihukumiwa miaka mitatu na nusu jela. Mwezi Agosti kabla ya kuachiwa huru mashitaka mapya ya ujasusi yalifunguliwa dhidi yake.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW