1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Niger waunga mkono hatua ya kufukuzwa balozi wa Ufaransa

27 Agosti 2023

Maelfu ya raia walikusanyika mjini Niamey kuunga mkono mapinduzi yaliyofanyika Niger mwezi uliopita pamoja na hatua ya kufukuzwa balozi wa Ufaransa.

Ufaransa imekuwa ikipingwa na kutakiwa kuondoka nchini humo tangu kulipofanyika mapinduzi ya kijeshi.
Raia wengi wa Niger wanauunga mkono utawala wa kijeshi nchini humo uliomuondoa madarakani Mohamed Bazoum.Picha: DW

Raia hao wa Niger walikusanyika katika uwanja mkubwa zaidi nchini humo wa Seyni Kountche wenye viti 30,000, uliojaa kwa theluthi mbili, huku bendera za Niger, Algeria na Urusi zikitawala.

Raia hao wanauunga mkono utawala mpya wa kijeshi ulioingia madarakani baada ya kumpindua rais Mohamed Bazoum.

Ijumaa, wizara ya mambo ya kigeni ya Niger ilitangaza kumtimua balozi wa Ufaransa Sylvain Itte kwa madai kwamba alikataa kukutana na watawala wapya. Iliongeza kuwa vitendo vya serikali ya Ufaransa vinakinzana na maslahi ya Niger.

Soma Pia: Niger yawatimua mabalozi wa nchi 4 ikiwemo Ujerumani