1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSri Lanka

Raia wa Sri Lanka wanapiga kura kumchagua rais

21 Septemba 2024

Huu ni uchaguzi wa kwanza tangu maandamano makubwa yaliyochochewa na mgogoro wa kiuchumi kufanyika na yaliyomuondoa madarakani Rais Gotabaya Rajapaksa mnamo mwaka 2022.

Sri Lanka I Colombo
Raia wa Sri Lanka wakishiriki zoezi la upigaji wa kura kwenye uchaguzi mkuu nchini humoPicha: Dinuka Liyanawatte/REUTERS

Raia wa Sri Lanka leo Jumamosi wanapiga kura ya kumchagua rais ajaye wa nchi hiyo iliyo kwenye mdororo mkubwa wa kiuchumi kuwahi kushuhudiwa.

Zaidi ya watu milioni 17 kati ya milioni 22 nchini humo wamejiandikisha kupiga kura katika uchaguzi wa urais ambao unaonekana kuwa wa ushindani kati ya Rais aliyeko madarakani Ranil Wickremesinghe,na kiongozi mkuu wa upinzani Sajith Premadasa na Anura Kumara Dissanayake anayeegemea siasa za mrengo wa kushoto.

Soma zaidi. Sri Lanka yafanya uchaguzi wa kwanza tangu maandamano yaliyomuondoa madarakani Rais Rajapaksa

Huu ni uchaguzi wa kwanza tangu maandamano makubwa yaliyochochewa na mgogoro wa kiuchumi kufanyika na yaliyomuondoa madarakani Rais Gotabaya Rajapaksa mnamo mwaka 2022.

Tayari zoezi hilo la upigaji kura limekwisha anza katika vituo mbalimbali nchini Sri Lanka na linatarajiwa kukamilika saa kumi jioni na kisha kufuata kwa zoezi la kuheshabiwa kwa kura
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW