Raia wa Syria ahukumiwa miaka 13 jela kwa jaribio la mauaji
5 Machi 2026
Matangazo
Shambulizi hilo lilifanyika katika makumbusho ya mauaji ya Holocaust huko mjini Berlin Februari 2025.
Mahakama hiyo imesema mshukiwa huyo mwenye umri wamiaka 20 ambaye ametajwa kwa jina la Wassim tu, amepatikana na hatia ya jaribio la mauaji na uanachama katika shirika la kigaidi.
Shambulizi hilo lililotokea Februari 2025 liliibua hisia kali wakatiambapo kulikuwa na mjadala mkali kuhusiana na uhamiaji, siku chache tu kabla uchaguzi mkuu.
Mshukiwa huyo alikiri kuwa alifanya tukio hilo kutokana na itikadi kali na kwa lengo la kidini.
Ujerumani ina karibu wahamiaji milioni moja kutoka syria, sehemu kubwa ya wahamiaji hao wakiwa waliingia mwaka 2015 wakati wa utawala wa Kansela Angela Merkel.