1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wa Syria washerehekea kuanguka utawala wa Assad

9 Desemba 2024

Raia wa Syria wamemiminika katika uwanja mkuu kwenye jiji la Damascus hii leo Jumatatu kuashiria mapambazuko yaliyokuwa yanasubiriwa kwa muda mrefu ya kuanguka kwa utawala wa Rais Bashar al-Assad.

Österreich Wien 2024 | Syrische Gemeinschaft feiert Sturz von Assad-Regime
Picha: Max Slovencik/APA/AFP/Getty Images

Assad alikimbilia Urusi jana Jumapili baada ya mashambulizi yaliyoongozwa na waasi walioudhibiti mji mkuu huo na hatimae kufungua ukurasa mpya katika historia ya Syria baada ya miongo mitano ya utawala wa ukoo wa Assad.  

Bashar al-Assad amepewa hifadhi nchini Urusi kutokana na kilichoelezwa kuwa sababu za kibinaadamu. Rais wa Marekani Joe Biden amesema ni lazima Assad awajibishwe kwa vitendo vya mauaji na mateso ya maelfu ya Wasyria.

Wakati huo huo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kufanya mkutano wa dharura na wa faragha ili kuijadili hali inayoendelea nchini Syria.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW