1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia waanza kuondoka Ukraine baada ya njia kufunguliwa

8 Machi 2022

Kumeripotiwa maendeleo kidogo katika uwekaji wa njia salaama kuwaruhusu raia kuepuka mapigano nchini Ukraine. Pande mbili zilikubaliana kusitisha mapigano kwa muda wa saa 12 siku ya Jumanne kupisha uhamishaji wa raia.

Ukraine-Krieg | Flucht aus Irpin bei Kiew
Picha: DIMITAR DILKOFF/AFP

Jeshi la Urusi limefahamisha kuwa kuwa limeanza kutekelea usitishaji mpya wa mapigano nchini Ukraine na kufungua njia za kiutu katika miji mitano.

Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Urusi Igor Konashenkov, alisema usitishaji mapigano umeanza asubuhi, na njia salaama zitafunguliwa kwa raia kutoka miji mikubwa ya Kyiv, Chernigov, Sumy, Kharkiv na Mariupol.

Soma pia: Mazungumzo ya Urusi, Ukraine yapiga hatua kidogo

Licha ya mapatano hayo, maafisa wa Ukraine wanasema ndege za Urusi zimeendelea kushambulia miji ya mashariki na kati mwa Ukraine usiku kucha. Makombora yalipiga viunga vya mji mkuu, Kyiv.

Kwa mujibu wa maafisa wa Moscow, sehemu kubwa ya njia hizo zitaelekea Urusi, ama moja kwa moja au kupitia Belarus.

Lakini Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa alisema njia za kiutu kutoka mji mkuu Kyiv na miji mingine zinaweza kuwapa watu chaguo la wapi wanataka kwenda.

Mwanaume akimsaidia mwanamek anaeondolewa kuvuka daraja lililoharibiwa wakati mwanamke huyo na wengine wakiondoka mjini Irpin, kaskazini-magharibi mwa Kyiv, Machi 7, 2022.Picha: DIMITAR DILKOFF/AFP

Maafisa wa Ukraine na Urusi walifanya duru ya tatu ya mazungumzo y amoja kwa moja jana Jamatatu, tangu kuanza kwa uvamizi Februari 24, na kwa mujibu wa wanadiplomasia wa mataifa hayo, mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa hayo mawili wanatarajiwa kukutana nchini Uturuki siku ya Alhamisi.

Zelenskiy kuteta na wabunge wa Uingereza

Rais Volodymyr Zelenskiy amewahimiza raia wake kuendelea kupinga uvamizi wa Urusi, ambao maafisa wa Umoja wa Mataifa wanasema umewalaazimisha watu zaidi ya milioni 1.7 kuikimbia nchi hiyo.

Soma pia:Maoni: Msaada wa NATO na Magharibi kwa Ukraine hautoshi 

Hii leo rais Zelenskiy atawahutubia wabunge wa Uingereza kupitia vidio, hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa rais wa taifa jengine kuhutubia bunge hilo kuu la Westminster.

Zelenskiy ambaye amezungumza mara kadhaa na waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson tangu uvamizi wa Urusi, ametoa hotuba kadhaa zilizovutia hisia kwa viongozi wa magharibi katika wiki iliyopita, akiwaomba vifaa na msaada wa kijeshi.

Picha iliiyotolewa na shirika la habari la serikali ya Urusi inaonyesha raia walioondolewa kwenye mji wa Mariupol.Picha: Erik Romanenko/Tass/dpa/picture alliance

Soma pia: Mazungumzo ya amani Ukraine yarejea

Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine anasema zaidi ya watu 20,000 kutoka mataifa 52 wamejitolea kupigana nchini Ukraine. Wakati vita hiyo ikiingia siku yake ya 13 hii leo, chakula, maji, joto la majumbani na dawa vimeendelea kuadimika nchini Ukraine.

Wakati huo huo, rais wa zamani wa UkraineViktor Yanukovych, alieko uhamishoni nchini Urusi, amemtaka Zelenskiy kusalimu amri, akisema anawajibika kusitisha umuagaji damu na kufikia makubaliano ya amani kwa gharama yoyote.

Raia wa Ukraine wazidi kukimbia nchi

02:21

This browser does not support the video element.

Yanukovych anaechukuliwa kuwa fisadi mkubwa, alipinduliwa na waandamanaji wanaolemea upande wa magharibi mwaka 2014, na alihukumiwa nchini Ukraine kifungo cha miaka 13 gerezani kwa makosa wa uhaini.

Vyombo vya habari nchini Ukraine viliripoti hivi karibuni kwamba ikulu ya Krelin inataka kumrejesha Yanukovych kama rais.

Chanzo: Mashirika