1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroJamhuri ya Kongo

Raia wakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula Goma

22 Februari 2024

Maelfu ya raia waishio kwenye mji wa GOMA mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya kongo, wanahangaika hivi sasa kutokana na upungufu mkubwa wa chakula ndani ya maduka na masoko ya eneo hilo.

DR Kongo | Mkaazi wa Goma
Mkaazi wa Goma Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoPicha: Cunningham/Getty Images

Hali hiyo inashuhudiwa baada ya waasi wa M23 kuzifungwa barabara muhimu zinazo sambaza bidhaa katika mji huo. 

Baadhi ya wakaazi wa mji huo wameamua kutumia njia ya maji kwenye ziwa kivu,wiki chache baada yakufungwa kwa barabara  za usambazaji wa chakula  kwenye mji wa Goma kutokana na vita vya M23.

Ziwa hilo linasalia kuwa njia pekee muhimu kwa kusafirisha  vyakula toka vijiji vya kivu kusini  hadi Goma kupitia mji mdogo wa Nzulo kilometa 18 kutoka  Goma kwenye mwambao wa ziwa kivu. 

Hata hivyo watu hao wanaoshuhudia ukosefu wa chakula kufuatia usalama mdogo kwenye barabara zinazokaliwa na waasi ,waelezea changamoto wanazozikabili wanapotumia njia hiyo mbadala.

"Hii ni njia mbaya sana sababu watu wanaweza kuzama ndani ya ziwa."  Alisema mmoja ya wakaazi wa mji huo ambao umeshuhudia mkururo wa mashambulizi kati ya,vikosi vya serikali ya Kongo na waasi wa M23.

Soma pia:Ombwe la uongozi DRC linaweza kuwapa nguvu waasi

Wakaazi hayo wanasema kwa wale wanaobahatika kupata bidhaa za chakula zimekuwa ni ghali kutokana na kile wananchokisema gharama ya usafirishaji.

"Idadi ya boti ni ndogo sana kulingana na uhitaji wa raia na hiyo imesababisha vyakula kutowasili kwa uwingi." Aliongeza mkaazi huyo.

Uchache wa vyombo vya usafiri wachangia

Hesabu ndogo ya boti za usafirishaji imekuwa pia ni jinamizi kubwa kwenye ziwa hilo,amesema bwana Maliro  Musemakweli ambae ni afisa wakiraia kwenye kijiji cha Nzulo.

"Kwa sasa tunapopata chakula kutoka Minova kupitia njia ya maji lakini bahati mbaya tumeorodha visa viwili vya watu wanao zama baada ya boti kupinduka ndani ya maji sababu kilo mtu anahitaji mzigo wake usafiri na hiyokusababisha ajali za mara kwa mara ".

Wakizungumza na DW, raia hao wanaohangaika kwa kutafuta chakula,wametaka serikali ya nchi hiyo kuingilia kati mara moja, na kumaliza adha hiyo ambayo imewagharimu idadi kubwa ya wakaazi ambao pia wanakabiliwa na kitisho cha usalama kutokana na mashambulizi ya waasi.

Maandamano ya kupinga ukosefu wa usalama yafanyika Goma

03:06

This browser does not support the video element.

Soma pia:UN yawawekea vikwazo waasi wa Kongo huku mapigano yakiendelea

Simwerayi Munyof mwenye kiti wa mashirika yakiraia eneo hilo la Nzulo, ameiomba mamalaka katika eneo hilo kufanya jitihada ili kufunguliwa kwa barabara.

"Tunaomba viongozi wetu kupata suluhu kwa tatizo hilo kwakupigana ili kufunguliwa  kwa barabara zote Muhimu. "

Karibuni wiki moja hivi sasa ,hali ya utulivu imeripotiwa kwenye mustari wa mapigano bain aya jeshi la kongo na waasi wa M23 ambao kulingana na vyanzo vya ndani ,ni kuwa waendelea kuonekana kwenye milima ya mji wa Sake ambamo raia wate wamekimbia. 

Kulingana na ripoti ya mataifa yakiratibu misaada ya dharura ,OCHA ilitangaza kuwa zatu zaidi ya watu milioni 6 wamekuwa wakimbizi  tangu mwaka uliopita na ambao sasa wanaathirika na tatizo hilo la ukosefu wa chakula katika makambi nje kidogo na mji wa Goma.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW