1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yadaiwa kuishambulia Kherson nchini Ukraine

2 Oktoba 2023

Gavana wa mji wa Kherson nchini Ukraine amesema mashambulizi ya usiku kucha ya Urusi mjini humo, yamesababisha mauaji ya mtu mmoja na kuwajeruhi wengine sita wakiwemo watoto wawili.

Rais Vladimir Putin haonyeshi nia ya kuumaliza uvamizi wake nchini Ukraine licha ya miito ya kimataifa
Rais Vladimir Putin haonyeshi nia ya kuumaliza uvamizi wake nchini Ukraine licha ya miito ya kimataifaPicha: Mikhail Metzel/Sputnik via REUTERS

Katika ujumbe wake katika mtandao wa kijamii wa Telegram, gavana Oleksandr Prokudin amesema wanajeshi wa Urusi wameshambulia mara 71 ndani ya saa 24 zilizopita na kulenga makaazi ya watu, maduka, vituo vya afya na maeneo mengine.

Hadi sasa Urusi haijatoa tamko lolote juu ya madai hayo.

Ukraine iliwaondoa wanajeshi wa Urusi nje ya mji wa Kherson mwezi Novemba mwaka jana baada ya kuudhibiti kwa miezi kadhaa.

Lakini bado wanajeshi wa Urusi wameendelea kuushambulia kutokea upande wa pili wa mto Dnipro unaonakatisha kwenye mkoa wa Kherson.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW