1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wanane wa waliuawa na walinda amani Kongo

9 Februari 2023

MONUSCO waliwauwa raia wanane walioushambulia msafara wa Umoja wa Mataifa jioni ya Jumanne wiki hii.

Demokratische Republik Kongo | MONUSCO Mission | Goma
Picha: Olivia Acland/REUTERS

Gavana huyo amesema raia hao waliuliwa ''kwa risasi za kutoa tahadhari'' zilizofyatuliwa na walinda amani wa MONUSCO, na kwamba wengine 28 walijeruhiwa.

Msafara wa MONUSCO ulishambuliwa na maelfu ya wakimbizi wa ndani, ulipofika eneo la Kanyaruchinya ukirejea mjini Goma.

MONUSCO haijatoa taarifa yoyote kuhusiana na mkasa huo. Raia wengi wa Kongo wamekuwa na hisia za chuki dhidi ya wanajeshi wa kigeni kwenye ardhi yao, wakiwashutumu kutazama tu wakati waasi wa M23 wakiendeleza mashambulizi  ambayo yamewalazimisha mamia kwa maelfu ya watu kuyahama makaazi yao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW