1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wanane wauawa nchini Mali

6 Januari 2025

Takriban raia wanane wameuawa katikati mwa Mali. Duru kadhaa zimeripoti juu ya mauaji hayo yaliyofanyika hapo jana Jumapili katika maeneo ya Niono na Nampala.

Mali Kati 2022 | Militärparade zum Armeetag vor Übergangspräsident Assimi Goita
Wanajeshi wa Mali wakifanya gwaride mbele ya wakuu wa serikali ya mpito wakati wa sherehe ya kuadhimisha siku ya kitaifa ya jeshi, Januari 20, 2022.Picha: Florent Vergnes/AFP/Getty Images

Duru hizo zimelilaumu jeshi la Mali na kundi la mamluki la Wagner la nchini Urusi kwa kuhusika na mashambulio hayo katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi inayokabiliwa na machafuko. Mali imekumbwa na mzozo wa kisiasa, kiusalama na kiuchumi, na tangu mwaka 2012 inakumbwa na mashambulizi ya makundi tofauti yenye mafungamano naAl-Qaeda na kundi inalojiita Dola la Kiislamu. Mali pia inakabiliana na waasi wanaotaka kujitenga katika jangwa la kaskazini mwa nchi hiyo. Jeshi la Mali lilichukua mamlaka katika mapinduzi ya mwaka 2020 na 2021 na tangu wakati huo limevunja uhusiano wake na Ufaransa katika kupambana na wapiganaji wenye msimamo mkali na kuamaua kuigeukia Urusi kisiasa na kijeshi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW