1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVisiwa vya Comoros

Raia wapiga kura kwenye visiwa vya Comoro

14 Januari 2024

Zoezi la kupiga kura linaendelea kwenye visiwa vya Comoro ambapo rais aliyemo madarakani Azali Assoumani anatarajiwa kushinda muhula wa nne.

Uchaguzi wa rais wafanyika Comoro
Uchaguzi wa rais wafanyika ComoroPicha: AFP/Getty Images/Y. Ibrahim

Watu wapatao laki tatu na arobaini elfu wamejiandikisha kupiga kura kwenye visiwa hivyo vyenye wakaazi laki nane.

Wapinzani wanadai kwamba tume ya uchaguzi inakipendelea chama tawala, madai ambayo tume hiyo imeyakanusha na imeeleza kuwa uchaguzi utafanyika kwa njia ya uwazi.

Rais Assoumani ambae hapo awali alikuwa afisa wa jeshi alitwaa madaraka mnamo mwaka 1999. Na tangu mwaka huo ameshinda katika chaguzi tatu.

Alishinda kwa kupata asilimia 60 ya kura katika uchaguzi wa mwaka 2019.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW