1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Uhalifu

Raia watatu wa China wahukumiwa kifungo cha miaka 7 DR Kongo

15 Januari 2025

Raia watatu wa China wamehukumiwa kifungo cha miaka saba jela na faini ya dola 600,000 kwa uchimbaji haramu wa madini katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

DRC Kongo | Mahakama | China | Dhahabu
Washtakiwa wakiwa mbele ya mahakama mjini Bukavu.Picha: Ernest Muhero/DW

Raia watatu wa China wamehukumiwa kifungo cha miaka saba jela na faini ya dola 600,000 kwa uchimbaji haramu wa madini katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Hatua hiyo imechukuliwa kwa mara ya kwanza dhidi ya madalali wa kigeni wa shughuli za uchimbaji madini kwa njia haramu katika taifa hilo. Wachina hao watatu pia walikutwa na hatia ya kufanya udanganyifu, utakatishaji pesa pamoja na uporaji.

soma pia: Wachina 17 wakamatwa Kongo kwa kuendesha mgodi haramu

Hata  hivyo, haijafahamika ikiwa washtakiwa hao wataendelea kubakia mjini Bukavu, mashariki mwa Kongo ambako wamezuiliwa au ikiwa watahamishiwa mahala kwengine.

Walikamatwa Januari 4 wakiwa na dhahabu pamoja na dola 400,000 pesa taslimu. Mawakili wanaowasimamia wamesema wanapanga kukata rufaa kupinga hukumu hiyo wanayosema, sio ya haki.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW