1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wawili wa Marekani wauwa Mexico

8 Machi 2023

Raia wawili kati ya 4 wa Marekani waliotekwa nyara katika eneo lililozongwa na uhalifu kaskazini mashariki mwa Mexico la Matamoros, wamepatikana wakiwa wamefariki dunia.

Mexiko Kidnapping, Amerikaner entführt
Picha: ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Raia wawili kati ya 4 wa Marekani waliotekwa nyara katika eneo lililozongwa na uhalifu kaskazini mashariki mwa Mexico la Matamoros, wamepatikana wakiwa wamefariki dunia. Taarifa hii imeipelekea Marekani kuahidi kuwachukulia hatua waliohusika katika tukio hilo.

Kulingana na mamlaka za Mexico, hao wawili wengine wamegunduliwa kwamba bado wapo hai baada ya kuvuka mpaka wa Mexico kutoka Marekani wakiwa wameelekea nchini humo kutafuta matibabu. Mexico hushuhudia mauaji ya makundi kihalifu na kufikia sasa zaidi ya watu laki tatu wameuwawa tangu serikali ilipotuma jeshi kupambana katika vita dhidi ya madawa ya kulevya mwaka 2006.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW