1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Raia wawili wauawa katika shambulizi la Urusi nchini Ukraine

15 Oktoba 2023

Mamlaka ya mkoa wa Donesk nchini Ukraine imesema leo kuwa raia wawili wameuawa katika shambulio la Urusi katika mji wa Mashariki wa Avdiivka hapo jana Jumamosi.

Moshi unafuka kutoka eneo kuelekea Avdiivka baada ya shambulizi la Urusi  mnamo Oktoba 11,2023
Moshi unafuka kutoka eneo kuelekea Avdiivka baada ya shambulizi la Urusi Picha: Alexnader Ermochenko/REUTERS

Katika ujumbe kupitia mtandao wa Telegram, mamlaka ya Donesk imesema mtu mwingine mmoja pia amejeruhiwa kwingineko katika eneo hilo.

Soma pia:Ukraine yasema imedungua ndege 28 za Urusi

Wakati huo huo, mkuu wa jeshi la Ukraine amesema leo kuwa vikosi vyake vilizuia mashambulizi 15 ya Urusi karibu na Avdiivka, Tonenke na Pervomaiske katika mkoa wa Donetsk, huku vikosi vya Urusi vikianzisha mashambulizi makali ya anga katika eneo hilo.

Urusi yafanya shambulizi la usiku kucha

Huku hayo yakijiri, Oleh Sinehubov, gavana wa eneo la Kharkiv ambalo pia liko Mashariki mwa Ukraine, amesema mwanamke mmoja wa umri wa miaka 54 na mwanamume wa umri wa miaka 57 waliuawa huku mwanamke mmoja akijeruhiwa katika shambulio hilo la anga la Urusi lililofanywa usiku kucha.

Soma pia:Mashambulizi ya Urusi yaua raia wawili wa Ukraine

Hata hivyo ripioti hizo hazikuweza kuthibitishwa.

Pande zote mbili zinakanusha kuwalenga raia katika vita hivyo ambavyo vilianzishwa na Urusi dhidi ya taifa jirani la Ukraine mnamo mwezi Februari mwaka jana.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW