1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIraq

Mashambulizi ya Uturuki yauwa wawili kaskazini mwa Iraq

8 Machi 2024

Watu wawili wameuwawa katika shambulizi la angani lililofanywa na Uturuki katika eneo lenye milima la Sheladiz katika mkoa wa kaskazini mwa Irak wa Duhok.

Mashambulizi ya Iraq dhidi ya Peshmerga na PKK
Mpiganaji aliyejeruhiwa akipelekwa hospitalini katika shambulizi ambalo wenzake watano walikufa huko Duhok, Iraqi Juni 05, 2021.Picha: Stringer/AA/picture alliance

Haya ni kwa mujibu wa vyanzo viwili vya usalama nchini Irak. Wizara ya ulinzi ya Uturuki imesema, usiku wa kuamkia leo, majeshi yake yamefanya mashambulizi kaskazini mwa Irak na Syria na kuwauwa wanamgambo sita nchini Irak na saba huko Syria. Wizara hiyo haikusema ni eneo gani lililolengwa na mashambulizi hayo na haijakuwa wazi iwapo ilikuwa inazungumzia shambulizi hilo hilo la kaskazini mwa Irak lililoripotiwa na vyanzo hivyo vya usalama Irak. KwakawaidaUturuki hufanya mashambulizi ya angani na operesheni za kuvuka mpaka wake nchini Irak, katika mashambulizi yanayolenga chama ilichokipiga marufuku cha PKK kilicho katika eneo la milimani la kaskazini mwa Irak.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW