1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raila Odinga akabidhi uongozi wa chama chake cha ODM

Angela Mdungu
12 Septemba 2024

Kinara wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amekabidhi uongozi wa chama cha ODM kwa gavana wa Kisumu Prof Peter Anyang Nyong'o.

Kinara wa upinzani Kenya Raila Odinga.
Kinara wa upinzani Kenya Raila Odinga.Picha: PHILL MAGAKOE/AFP

Nyong'o ataongoza kama kaimu Mwenyekiti wa ODM kipindi hiki ambapo Odinga ametangaza kuachana na  siasa za ndani ya nchi ili kushugulikia kinyanganyiro cha uenyekiti wa Umoja wa Afrika.

Taarifa ya uteuzi wa Nyongo imetolewa na katibu mkuu wa sasa wa chama hicho cha ODM, Edwin Sifuna. 

Soma pia:Ruto awateua vigogo wanne wa upinzani katika baraza la mawaziri

Kiongozi wa ODM atatangazwa rasmi, baada ya matokeo ya uchaguzi wa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ifikapo Februari mwaka 2025 kwa kutegemea kwamba Odinga atatangazwa kuwa ni mwenyekiti mpya iwapo atakuwa ameshinda kinyang'anyiro hicho. 
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW