1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raila Odinga kuzikwa baadaye leo kwao Siaya, Bondo

19 Oktoba 2025

Hafla ya mazishi ya aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga inaendelea nyumbani kwake Siaya Bondo huku kukiwa na ulinzi mkali kufuatia vurugu mbaya zilizotokea katika mji mkuu wa nchi hiyo wakati wa ibada ya kitaifa.

Kenya Bondo 2025 | Raila Odinga azikwa Siaya, Bondo
Ibada ya mazishi ya aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya, Raila OdingaPicha: Musa Naviye/DW

Odinga, anayetajwa kuwa mwanaharakati wa demokrasia, ametunukiwa heshima kamili ya kijeshi pamoja na taratibu za kitamaduni na atazikwa karibu na kaburi la baba yake.

Odinga, aliyekuwa na umri wa miaka 80, alifariki dunia Jumatano nchini India, na mwili wake kurejeshwa nchini Kenya siku ya Alhamisi .

Hafla nne za kutazama mwili wa Raila zimeandiliwa katika muda wa siku tatu zilizopita na kuwavutia maelfu ya waombolezaji pamoja na kusababisha vifo vya watu watano na kujeruhiwa kwa mamia ya wengine kwenye makanyagano yaliotokea.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW