1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Abaas wa Palestina azungumza na Wolfensohn

30 Julai 2005

Gaza:

Rais wa Palestina, Mahmud Abbas, ameanza mazungumzo leo na Mjumbe wa pande nne wa Mashariki ya Kati James Wolfensohn. Mazungumzo yao yanahusu uchumi wa siku zijazo wa Ukanda wa Gaza baada ya Waisraeli kuondoka katika sehemu hiyo. Msemaji wa Rais, Nabil Abu Rudeina, amesema kuwa Rais Abbas ameanza kuzungumza na Bw. Wolfensohn kuhusu ujenzi mpya wa miundo mbinu iliyoharibiwa na Waisraeli katika Ukanda wa Gaza baada ya kuondoka kwao. Mazungumzo yao yatajishughulisha pia na msaada wa Dollar Billioni tatu ulioahidiwa kutolewa na kikundi cha nchi nane zilizoendelea kiviwanda kinachojulikana kama G8 wakati wa mkutano wao mapema mwezi huu. Bw. Wolfensohn atakutana pia na Waziri wa Huduma za Jamii, Mohammad Dahlan.