SiasaMamlaka ya Palestina
Kiongozi wa Palestina amteua Waziri Mkuu mpya
15 Machi 2024Matangazo
Mustafa anateuliwa wiki mbili baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu Mohammad Shtayyeh kujiuzulu na serikali yake akiangazia mabadiliko katika Ukanda wa Gaza.
Mwanauchumi huyo ambaye ni mjumbe wa tume huru tendaji ya Chama cha Ukombozi wa Wapalestina PLO, amewahi pia kuwa naibu waziri wa masuala ya uchumi na mjumbe wa Wakfu wa Uwekezaji wa Palestina.
Mwanasiasa huyo, 69 sasa anakabiliwa na jukumu la kuunda serikali mpya ya Mamlaka ya Palestina, yenye ushawishi hafifu katika maeneo ya Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na Israel.
Tangu mwaka 2007, kumekuwa na mgawanyiko wa udhibiti wa maeneo ya Palestina. Wakati Ukingo wa Magharibi ukitawaliwa na serikali ya Abbas, Gaza iko chini ya kundi la Hamas.