1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAzerbaijan

Rais Aliyev asema Russia ilidungua ndege ya nchi yake

29 Desemba 2024

Rais wa Azerbaijan lham Aliyev asema ndege ya nchi yake iliyopata ajali Disemba 25, ilidunguliwa na Urusi, kwa bahati mbaya.

Ndege ya abiria ya Azerbaijan ilidunguliwa na Russia
Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev akihojiwa na kituo cha televisheni cha AzerbaijanPicha: President of Azerbaijan Ilham Aliyev via REUTERS

Kiongozi huyo pia ameikosoa Urusi kwa kujaribu "kuficha" ukweli juu ya suala hilo kwa siku kadhaa.

Ameiambia televisheni ya taifa ya Azerbaijan kwamba, amesikitishwa na wakati huo huo kushangazwa na sababu zilizotolewa na maafisa wa Urusi kuhusu chanzo cha ajali hiyo.

Ajali hiyo ya ndege iliyotokea Disemba 25, ilisababisha vifo vya watu 38 kati ya 67 waliokuwemo kwenye ndege hiyo.

Ikulu ya Urusi, Kremlin, ilisema mifumo yake ya ulinzi ya anga ilikuwa ikifyatua makombora karibu na Grozny, mji mkuu wa Chechnya, eneo ambalo ndege hiyo ilijaribu kutua, ili kuzuia shambulio la droni la Ukraine.

Rais wa Urusi Vladimir Putin tayari amemuomba msamaha Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev japo hakukiri moja kwa moja kwamba Moscow ilihusika na ajali hiyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW