1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa kikanda kujadili mzozo wa Afghanistan

15 Julai 2021

Rais wa Afghanistan, Ashraf Ghani anakutana na viongozi wa kikanda nchini Uzebekistan katika kipindi hiki ambacho hali ya usalama nchini mwake imezidi kuzorota. Hofu imetanda kuhusu uwezekano wa wakimbizi wa Afghanistan.

Afghanistan | Taliban
Picha: Hoshang Hashimi/AFP/Getty Images

Kwa mujibu wa Shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR, mamilioni ya watu wameachwa bila wa makazi kutokana na vita hivyo vya miaka kadhaa, wakiwemo 270,000 katika mapigano ya tangu Januari, wakati huu ambapo vikosi vya kigeni vinavyoongozwa na Marekani vikiwa katika hatua za mwisho za kujiondoa kabisa nchini Afghanistan.

Wakati wapiganaji wa Taliban wakidhihirisha nia yao ya kuishinda serikali ya Ghani, yenye kuungwa mkono na mataifa ya Magharibi, mataifa jirani na Afghanistan yapo katika hali ya tahadhari kuhusu wakimbizi wanaovuka mipaka, huku mapigano yakipamba moto na hali ya maisha ya kawaida ikizidi pia kuzorota. Mwanadiplomasia mmoja aliyenukuliwa na Shirika la Habari la Uingereza la Reuters amesema mkutano huo wa siku mbili unaofanyika mjini Tashkent utajikita juu ya hatma ya baadae ya Afghanistan na kuhusisha suluhu ya kidiplomasia.

Hatma ya Afghanistan na ustawi wa diplomasia ni ajenda muhimu.

Rais Ashraf Ghani na ujumbe wakePicha: Presseabteilung des Präsidenten von Afghanistan

Mmoja wa wajumbe wa mkutano huo Sirojiddin Muhriddin ni  Waziri wa Mambo ya Nje wa Tajikistan. anasema "Mataifa wanachama wa ushirikiano wa Shanghai (SCO) yanaunga mkono jitihada za serikali na watu wa Afghanistan za kurejesha amani, maendeleo ya uchumi ya taifa,kukabiliana na ugaidi, itikadi kali na uhalifu wa biashara haramu ya dawa za kulevywa."

Vita hivyo vya miongo kaadha vimewasababisha raia wa Afghanistan kulikimbia taifa lao na wengi wao wameingia matiafa jirani ya Pakistan kwa mashariki na upande wa magharibi Iran.

Pakistan na Iran ndio zenye idadi kubwa ya wakimbizi.

Pakistan kwa mfano, ndio pamekuwa nyumbani kwa wakimbizi milioni 1.4, wakati Iran inawahifadhi karibu milioni moja kulingana na data za shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa kuanzia mwaka huu. Lakini idadi ya Wafghanistani wasioandikishwa katika mataifa yote mawili ni kubwa zaidi.

Katika hatua nyingine kiongozi wa timu ya upatanishi wa Afghanistan, Nader Nadery amesema Taliban imejitolea kuweka chini mtutu wa bunduki kwa miezi mitatu kwa makubaliano ya kuacchiwa huru wafungwa 7,000, wapiganaji ambao wanashikiliwa na serikali ya Afghanistan. Kauli hiyo inatolewa wakati wapiganaji wa kundi hilo wakiendelea na mashambulizi makali yenye kuambatana na udhibiti wa maeneo mengi.

Tangazo hilo ambalo amelitoa wakati walinzi wa Afghanistanwakitumia mabomu ya machozi kuwatawanya raia wa taifa hilo wanaotaka kuvuka mpaka kukimbia machafuko na kuingia Pakistan linasema Taliban inataka kuondolewa viongozi wake katika orodha mbaya ya Umoja wa Mataifa.

Vyanzo:AFP/RTR

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW