Rais Azali anaendelea vyema baada ya kushambuliwa kwa kisu
14 Septemba 2024Maafisa nchini Komoro wamesema kuwa Rais Azali Assoumani "hayuko hatarini" baada ya kujeruhiwa siku ya Ijumaa kwa kisu na polisi mwenye umri wa miaka 24, ambaye baadaye alipatikana amekufa.
Shambulio hilo lilitokea mwendo wa saa 2 usiku kwa saa za Komoro hapo jana katika mji wa Saliamani Itsandra ulioko kaskazini mwa mji mkuu, Moroni.
Soma zaidi. Rais wa Comoro Azzali Assoumani ampatia mwanae wa kiume wadhifa serikalini
Waziri wa Nishati Aboubacar Said Anli akizungumza na waandishi wa habari amewatoa hofu Wakomoro kwamba Rais Azali anaendelea vyema.
Mtuhumiwa wa mashambulizi hayao, aliyefahamika kwa jina la Ahmed Abdou, alikuwa ameenda likizo siku ya Jumatano kabla ya kupanga kufanya tukio hilo siku ya Ijumaa.
Polisi inasema mtuhumiwa huyo amekutwa amefariki katika eneo alimokuwa amewekwa chini ya uangalizi kwa uchunguzi.