1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Barrak Obama- majeshi ya Marekani kuondoka Iraq.

Eric Kalume Ponda21 Januari 2009

Bado shamra shamra za kumkaribisha rais mpya wa Marekani Barrak Obama zinaendelea huku viongozi wa mataifa mbali mbali ulimwenguni wakiendelea kumlimbikizia sifa tele rais huyo kwenye risala zao za pongezi.

Rais Barrak ObamaPicha: AP

Rais Barrak Obama ameanza safari ndefu kutekeleza ahadi alizozitoa wakati wa kampeini huku jamii ya kimataifa ikisubiri kwa hamu kuona matumaini yao kuunganisha na kuleta amani kote ulimwengu yakitimia.


Hapana shaka rais Barrak Obama ataingia katika kumbu kumbu sio tu kama rais wa kwanza Mmarekani mweusi kuliongoza taifa hilo kubwa ulimwenguni, bali kutokana na sera zake zilizoinua matumaini ya wengi .


Rais Barrak Obama anafahamu fika jukumu kubwa lililoko mbele yake, na ndio maana hajapoteza muda kufungua ukurasa kushughulikia majukumu aliyokabidhiwa. Ajenda kuu ikiwa amani na kudumishwa demokrasia kote ulimwenguni, na ndio maana hakusita wakati wa kuapishwa kwake kuwaonya viongozi wanaoendeleza ubabe katika mataifa mengi ya Ulimwengu.


Lakini kabla ya kuanza shughuli zake hii leo rais Barrak Obama alihudhuria misa ya kuomba baraka katika kanisa la Cathedral mjini Washington.


Kisha akatoa agizo la kuahirishwa kwa muda wa siku 120 kusikizwa kwa mashtaka yanayowakabili watuhumiwa 254 wanaozuiliwa katika Gezera la Guantanamo.


Zaidi ya watuhumiwa 800,wake kwa waume vijana kwa wazee wamepitia gereza hilo,lililofunguliwa Januari 11 mwaka wa 2002.


Viongozi wa mashtaka wanatarajiwa kutoa uamuzi wao kuhusiana na agizo hilo ambalo ni pamoja na kusimamishwa kwa mshtaka yanayowakabiliwa watuhumiwa 5 wa shambulio la septemba 11 mwaka wa 2001 nchini Marekani.


Suala la pili ambalo limemkosesha usingizi rais Barrak Obama ni vita vya Iraq, na leo hii baada ya kukutana na maafisa wakuu wa kijeshi aliwaagiza kuandaa mpango wa kuyaondoa majeshi ya Marekani nchini humo.


Kwa kuzingatia hotuba aliyoitoa jana wakati wa kuapishwa, hatua hiyo ni ya kujenga uhusiano bora na wala isichukuliwe kuogopa,akionya mataifa ya kiarabu na ulimwengu kwamba hamuwezi kutudhiofisha na tutawashinda.


Hali kadhalika uchumi wa Marekani ni miongoni mwa masuala aliyoyashughulikia hivi leo na Rais Obama, baada ya kukutana na washauri wakuu wa masuala ya kiuchumi ili kutafuta njia za kuurejesha uchumi wa taifa hilo katika mkondo ufaao.


Kamati hiyo ya ushauri inapendekeza kwa bunge la Marekani kuidhinisha kiasi cha dola bilioni 825 kufufua uchumi wa taifa hilo.


Ponda/Reuters















Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW