1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden akutana na mwenzake wa Poland na kuahidi mshikamano

21 Februari 2023

Rais wa Marekani Joe Biden amekutana na mwenzake wa Poland Andrzej Duda mjini Warsaw leo na kusisitiza dhamira ya Washington ya kuhakikisha usalama barani Ulaya katikati mwa kitisho kinachoongeza kutoka Urusi.

Polen | Joe Biden und Andrzej Duda
Picha: JANEK SKARZYNSKI/AFP/Getty Images

Akihutubia mkutano na waandishi habari baada ya mazungumzo yake na rais Duda, Biden amesema bara la Ulaya ni lazima libakie kuwa salama na mshikamano wa mataifa ya magharibi umezidi kuimarika tangu Urusi ilipoanzisha vita nchini Ukraine.

Kwa upande wake rais Duda ameusifu msimamo wa Biden ikiwa ni pamoja na ziara aliyoifanya jana mjini Kyiv kuonesha mshikamano na  Ukraine.

Baadaye leo jioni rais Biden atatoa hotuba inayotarajiwa kuzungumzia pamoja na mambo mengine msimamo usioyumba wa mataifa ya magharibi katika kuiunga mkono Ukraine kwenye vita dhidi ya Urusi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW