1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Rais Biden kufanya ziara fupi nchini Ujerumani wiki ijayo

13 Oktoba 2024

Rais wa Marekani Joe Biden anatarajiwa kufanya ziara ya siku moja nchini Ujerumani Ijumaa ya wiki ijayo.

Rais wa Marekani Joe Biden (kushoto) akiwa na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz
Rais wa Marekani Joe Biden (kushoto) akiwa na Kansela wa Ujerumani Olaf ScholzPicha: Elijah Nouvelage/UPI Photo via Newscom/dpa/picture alliance

Rais Biden atakutana na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na Rais Frank-Walter Steinmeier. Hii ni baada ya kuifuta safari yake iliyokuwa imepangwa wiki hii kutokana na kimbunga Milton kilichopiga jimbo la Florida.

Ziara ya awali ya Biden nchini Ujerumani ilikuwa ifanyike kati ya Oktoba 10 na 12 ambapo angelikutana na Scholz, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer.

Pia alikuwa amepanga kufanya mkutano na zaidi ya washirika 50 wa Ukraine katika  kambi ya Ramstein  ili kujadili uungaji mkono zaidi kwa Kyiv katika mapambano yake dhidi ya uvamizi wa Urusi na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alitarajiwa kuhudhuria mkutano huo. 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW