1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Rais Biden atoa rai kupitishwa mageuzi ya idara za polisi

3 Februari 2023

Rais wa Marekani Joe Biden amesema ana matumaini kwamba kifo cha kijana wa kimarekani Tyre Nichols kilichotokana na kipigo cha polisi kitashinikiza bunge kuidhinisha mageuzi ya uendeshaji idara za polisi nchini humo.

US-Präsident Joe Biden
Picha: Drew Angerer/Getty Images

Akizungumza kwenye mkutano uliofanyika ikulu ya White House kati yake na kundi la wabunge weusi siku moja baada ya mazishi ya Nichols, rais Biden amesema anaamini mkasa huo utachochea wabunge kuona umuhimu wa kuchukua hatua kukomesha matendo ya aina hiyo.

Tyre Nichols, mmarekani mweusi mwenye umri wa miaka 29 aliaga dunia mjini Memphis mnamo Januari 10, siku tatu baada ya kushambuliwa vibaya na polisi waliomsimamisha kwa ukaguzi wa usalama barabarani.

Kifo chake kimezusha hasira miongoni mwa wamarekani na kuibua upya mjadala juu ya mageuzi katika idara za polisi ambayo chama cha rais Biden kimejaribu kuyapitisha bungeni bila mafanikio tangu mwaka 2020.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW