1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNigeria

Rais Bola Tinubu alibadilisha baraza la mawaziri

24 Oktoba 2024

Rais wa Nigeria Bola Tinubu amewafukuza kazi mawaziri watano na kuwateua wapya saba katika mabadiliko ya baraza la mawaziri.

Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu
Rais wa Nigeria Bola Tinubu akizungumza kwenye ufunguzi wa Jukwaa la Ushirikiano wa China na Afrika, FOCAC, huko mjini Beijing, Septemba 5, 2024Picha: Greg Baker/AP Photo/picture alliance

Kulingana na ofisi ya Rais Tinubu, miongoni mwa walioteuliwa ni waziri wa masuala ya kibinadamu na kupunguza umaskini, biashara na uwekezaji, kazi na maendeleo ya mifugo.

Tinubu pia amewabadilisha mawaziri wengine 10, katika mabadiliko yanayolenga kuleta ufanisi zaidi kwenye serikali yake.

Mabadiliko haya aidha yanafanyika katikati ya hali mbaya ya kiuchumi, hali iliyochochea maandamano yaliyozimwa kwa gesi ya kutoa machozi.

Aidha, Wizara ya Maendeleo ya Niger Delta imebadilishwa jina na kuwa Wizara ya Maendeleo ya Kanda, huku Wizara za Michezo utalii, sanaa na utamaduni zikiunganishwa na kuwa wizara moja.