1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Buhari kusaini muswada mpya wa bajeti kukabili corona

10 Julai 2020

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari kutia saini muswada wa sheria ya bajeti iliyorekebishwa ya dola za kimarekani bilioni 28.38.

Nigeria Abuja Präsident Muhammadu Buhari
Picha: picture-alliance/dpa/W. Krumm

Bajeti hiyo ilipitishwa na bunge mwezi Juni baada ya kurekebishwa, katika juhudi za serikali kukabiliana na athari za kiuchumi zilizosababishwa na janga la Corona na pia kushuka kwa bei ya mafuta.

Waziri wa fedha Zainab Ahmed jana Alhamisi pia alifanya mazungumzo na wabunge na kutoa utaratibu wa mipango ya serikali wa utumiaji wa fedha, mipango ambayo anapanga kuiwasilisha bunge baadaye mwezi huu.

Nchi hiyo ndiyo mzalishaji mkubwa wa mafuta barani Afrika, na inategemea zaidi mauzo ya mafuta ghafi yanayochangia karibu asilimia 90 ya mapato ya kigeni.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW