1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Chavez atuma helikopta kuchukuwa mateka Colombia

29 Desemba 2007

VILLAVICENCIO

Rais Hugo Chavez wa Venezuela ametuma helikopta nchini Colombia hapo jana kuwachukuwa mateka watatu akiwemo mvulana aliezaliwa wakati wakishikiliwa mateka kwa miaka chungu nzima na waasi wa Kimarxisti kwenye kambi za vichakani.

Helikopta hizo mbili zimewasili kwenye mji wa Villavicencio ulio kame chini ya milima ya Andes nchini Colombia hapo jana mchana na zitaruka kwenda kuwachukuwa mateka hao wakati zitakapoashiriwa kufanya hivyo na watekaji wao.

Akizungumza kwenye kambi ya kijeshi nchini Venezuela wakati helikopta hizo zilipokuwa zikiondoka kuelekea Colombia Chavez amesema operesheni hiyo kuu ya uokozi imecheleweshwa hadi mwishoni mwa juma kutokana na waasi kutomweleza mahala gani wanashikiliwa mateka hao.