1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Chiluba wa Zambia aitwa kujieleza mbele ya kitengo cha kupambana na Rushwa.

25 Machi 2008

Lusaka.

Rais wa zamani wa Zambia Frederick Chiluba ametakiwa kufika siku ya Alhamis mbele ya kitengo maalum cha uchunguzi kuhusu rushwa kitendo kilichotokea chini ya utawala wake.

Chiluba amepokea waraka huo unaomtaka kufika mbele ya kitengo hicho leo Jumanne mjini Lusaka , siku moja baada ya kurejea kutoka Afrika kusini ambapo alikuwa kwa matibabu ya matatizo ya kupumua.

Chiluba ambaye tayari anakabiliwa na madai kadha ya ufisadi mahakamani, anashutumiwa kwa kuiba kiasi kikubwa cha fedha za umma pamoja na watu wake wa karibu na maafisa wakati wa utawala wake wa miaka 10.

Kiongozi huyo wa zamani amekana madai hayo, akisema kuwa kukamatwa kwake kuna ushawishi wa kisiasa kutoka kwa kiongozi aliyeko madarakani hivi sasa Levy Mwanawasa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW