China na Urusi zalaani mpango wa Marekani wa kuweka makombora ya ulinzi ...
23 Mei 2008Rais Dmitry Medvedev wa Urusi na kiongozi wa China Hu Jintao wamelaani mpango wa Marekani wa kuweka ulinzi wa makombora katika nchi za Ulaya ya mashariki.
Katika tamko la pamoja mjini Beijing baada ya rais Medvedev kuwasili China leo viongozi hao wamesema mpango huo utarudisha nyuma juhudi za kupunga silaha.
Katika tamko hilo China na Urusi zimesema mpango wa Marekani wa kuweka mtandao wa kimataifa wa ulinzi dhidi ya makombora hautasaidia kudumisha urari wa nguvu za kijeshi na wala hautasaidia kuimarisha taratibu za kuzuia uenezaji wa silaha za nyuklia.
Rais Dmitry Medvedev wa Urusi amewasili nchini China kuanza ziara ya kwanza katika nchi za nje tokea aapishwe kuwa rais wa Urusi.
Ziara ya siku mbili ya rais Medvedev nchini China ila lengo la kuimarisha ushirikiano katika sekta za kijeshi na nishati. Na kwa ajili hiyo nchi hizo zimetiliana saini mapatano juu ujenzi wa kinu cha kuzalisha nishati ya nyuklia.
Mtambo huo utajengwa kwa thamani ya dola za kimarekani bilioni moja.