1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump aahidi kuwa rais atakayeleta amani

21 Januari 2025

Rais mpya wa Marekani aliyeapishwa jana, amesema anataka kuweka sifa ya kuwa mmoja wa viongozi watakaoleta amani na mshikamano.

Rais Donald Trump
Rais Donald Trump aahidi kuwa rais atakayeleta amani na mshikamano baada ya kuapishwa kuiongoza tena MarekaniPicha: Jim Watson/AFP/Getty Images

Katika hotuba ya kuapishwa kwake, Trump alizungumzia kuridhishwa kwake na hatua ya kuachiliwa huru kwa mateka wa Israel na wafungwa wakipalestina chini ya makubaliano ya usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza.

Rais Samia athibitisha maambukizi ya Marburg nchini Tanzania

Baada ya hafla ya kuapishwa,Trump  alishiriki kwenye sherehe za gwaride zilizoandaliwa kumkaribisha na kusaini amri  kadhaa za rais pamoja na kutoa msamaha kwa wafuasi wake waliovamia majengo ya bunge Januari 6 mwaka 2021.

Viongozi mbali mbali wakiwemo wa nchi za kiarabu wametuma salamu zao za kumpongeza rais huyo mpya wa Marekani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW