SiasaChina
Rais Trump awasili Beijing kwa mazungumzo na Xi
13 Mei 2026
Matangazo
Trump alikaribishwa na Makamu wa Rais wa China Han Zheng, pamoja na maafisa wengine waandamizi wa serikali, balozi wa China nchini Marekani na mjumbe wa Washington mjini Beijing, David Perdue.
Mazungumzo muhimu ya mkutano huo wa kilele yatafanyika kesho wakati viongozi hao wawili watakapotembelea eneo ambako watawala wa China walikuwa wakiombea mavuno na ambako kulifanyika dhifa za kitaifa, linalojulikana kama Temple of Heaven.
Pamoja na suala la Iran, serikali ya Trump inatarajia kuanzisha Bodi ya Biashara na China itakayoshughulikia tofauti baina ya mataifa hayo mawili.