Rais Emmanuel Macron aanza ziara nchini Madagascar
23 Aprili 2025
Matangazo
Ziara hiyo ya Macron inalenga kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizo mbili pamoja na kuendelea kuimarisha uwepo wa Ufaransa katika eneo hilo la Bahari ya Hindi, licha ya kuwepo mivutano inayoendelea ya enzi ya ukoloni.
Ni ziara ya kwanza rasmi ya kiongozi wa Ufaransa nchini Madagascar tangu ile iliyowahi kufanywa mwaka 2005 na Jacques Chirac.
Rais Macron aliyeandamana kwenye ziara hiyo na mkewe Brigitte atakuwa na mikutano na Rais Andry Rajoelina na viongozi wa kibiashara mjini Antananarivo.