1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais George W.Bush amewasili nchini Benin

16 Februari 2008

COTONOU:

Rais wa Marekani George W.Bush amewasili nchini Benin akianza ziara yake ya siku sita barani Afrika.Ziara hiyo itamfikisha pia nchini Tanzania,Rwanda,Ghana na Liberia.Kwa mujibu wa Washington,mada kuu katika ajenda ya Rais Bush ni mageuzi ya kidemokrasia,misaada ya kijeshi na miradi ya Marekani kupiga vita magonjwa kama UKIMWI na malaria.

Hadi hivi sasa,Liberia ni nchi pekee iliyokuwa tayari kuiruhusu Marekani kuwa na makao makuu ya kikosi chake kwa ajili ya Afrika kiitwacho AFRCOM.Bush anatazamiwa pia kujadili mzozo wa hivi sasa nchini Kenya na mgogoro wa Darfur.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW