Rais Hamid Karzai aongoza kwa mara ya pili
17 Septemba 2009Matangazo
Kulingana na waangalizi wa uchaguzi wa Umoja wa Ulaya walioko nchini Afghanistan kiasi cha kura milioni 1.5 huenda zilikuwa na hila.
Kulingana na matokeo ya muda yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Afghanistan baada ya kuzihesabu upya baadhi ya kura zilizopigwa Rais Hamid Karzai amepata takriban asilimia 55 ya kura zote.Mpinzani wake mkuu Abdullah Abdullah anaripotiwa kuwa amepata kiasi cha asilimia 28 ya kura zote.Hali hiyo imeifanya Tume ya Uchaguzi inayohusika na matatizo ya uchaguzi imeamrisha kiasi cha asilimia 10 ya kura zote kuhesabiwa upya.
Thelma Mwadzaya/ AFPE,DPAE