Rais Herzog kuzingatia nchi kwanza kuhusu ombi la Netanyahu
1 Desemba 2025
Matangazo
Kwenye taarifa yake, Herzog amesema suala hilo litazingatiwa kwa njia sahihi kabisa, na kwamba ataongozwa na masilahu muhimu ya nchi ya Israel atakapotoa uamuzi.
Netanyahu alitangaza siku ya Jumapili kwamba amewasilisha rasmi ombi la kutaka msamaha wa rais akisema kesi hizo zinazidi kuigawa Israel.
Rais wa Marekani Donald Trump pia alimuandikia barua Rais Herzog akimsihi amsamehe Netanyahu, ambaye mara kwa mara amekanusha mashtaka dhidi yake.
Netanyahu na mkewe wanakabiliwa na mashtaka ya kukubali bidhaa za thamani ya zaidi ya dola 260,000 kama rushwa.