1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Jacques Chirac wa Ufaransa awatanabahisha raia juu ya umuhimu wa umoja wa Ulaya

15 Aprili 2005

Paris

Rais Jacques Chirac wa Ufaransa amewatahadharisha raia wa nchi hiyo dhidi ya kuipinga katiba ya ulaya kura ya maoni itakapoitishwa may 29 ijayo.Kiongozi huyo wa Ufaransa amesema pindi kura ya la ikishinda basi utaratibu mzima wa muungaano wa ulaya utaparaganyika.Ulaya iliyoungana na yenye nguvu ni kwa masilaha ya Ufaransa pia,amesema kiongozi huyo wa Elysée.Katika mahojiano kwa njia ya televisaheni pamoja na vijana wenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 30,rais Jacques Chirac ameondowa uwezekano wa kujiuzulu pindi kura ya la ikiishinda.Utafiti wa maoni ya umma nchini Ufaransa umeonyesha asili mia 55 ya wapiga kura wa Ufaransa wataipinga katiba ya Umoja wa Ulaya,kura ya maoni itakapoitishwa mwishoni mwa mwezi ujao.